1. MAELEZO MAFUPI KUHUSU MADHUMUNI YA SOMO.

 Lengo kuu la moduli hii ni kuwapatia wanafunzi elimu kuhusu fasihi simulizi na fasihi andishi katika lugha ya Kiswahili. Yaliyomo katika moduli hii yanahusu pia sifa na dhima za fasihi simulizi na tanzu zake mbalimbali kuhusu fasihi simulizi na uchambuzi wa baadhi ya kazi za sanaa. 


a. MALENGO MAKUU YA SOMO


A. Ujuzi na ufahamu:


Mwanafunzi atakayeshinda moduli hii ni yule ambaye atakuwa anaonyesha ujuzi na ufahamu wa mambo yafuatayo:

i. Kiwango cha fasihi simulizi katika lugha ya Kiswahili, tanzu za fasihi simulizi, dhima za fasihi simulizi na matatizo yanayoandamana na historia ya fasihi ya Kiswahili pamoja na uhakiki wa fasihi hii.

ii. Fasihi simulizi na matatizo yanayolandana nake: katika usimuliaji wake, usaambazaji na uhifadhi wake na kufanyiwa utafiti.

iii. Vipengele vya ushairi wa Kiswahili kulingana na historia ya Afrika ya Mashariki: kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni.

iv. Tanzu za ushairi na Washairi maarufu na kazi zao muhimu.


B. Ujuzi kimatumizi:

Mwanafunzi atakayekuwa ameshinda moduli hii ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa:

i. Kufahamu tanzu mbalimbali za fasihi simulizi na fasihi andishi katika lugha ya Kiswahili

ii. Kutathmini hali ya fasihi simulizi na fasihi andishi

iii. Kutumia elimu na ujuzi katka uchambuzi wa kazi mbalimbali za fasihi simulizi katika lugha ya Kiswahili.


C. Ujuzi kimatendo:

Mwanafunzi atakayekuwa ameshinda moduli hii ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa:

i. Kutumia vizuri na kwa uangalifu ujuzi alioupata katika utumiaji wa fasihi ya Kiswahili.

ii. Kuchunguza matini na vyombo vya habari tofauti katika wakati wa kuichunguza fasihi ya Kiswahili.

iii. Kutumia marejeo kwenye intaneti wakati wa utafiti kuhusu mambo ya fasihi.


2. YATAKAYOFUNDISHWA KATIKA MODULI HII:


Msisitizo utawekwa kwenye mambo yafuatayo:

1. Fasili na dhana ya fasihi simulizi 

2. Sura na mawanda vya fasihi simulizi 

3. Dhima ya fasihi simulizi kwa jamii ya Afrika ya leo 

4. Tanzu za fasihi simulizi.

5. Fasihi simulizi na matatizo yanayolandana nake

6. Fasili na usuli wa ushairi wa Kiswahili 

7. pengele vya ushairi wa Kiswahili kulingana na historia ya Afrika ya Mashariki: 

a. Kabla   ya ukoloni, 

b. Wakati wa ukoloni 

c. Baada ya ukoloni 

8. Fani na  maudhui katika ushairi wa Kiswahili


9. Uchambuzi wa kazi mbalimbali za fasihi: riwaya, tamthilia na ushairi.




















10. MBINU ZA UFUNDISHAJI NA USOMAJI

Kazi za mazoezi na mtihani wa mwisho vitapewa wanafunzi kwa ajili ya kuchunguza iwapo malengo yaliyotarajiwa katika moduli hii  yatakuwa yamefikiwa. Kazi ndogo ndogo huwa zinapewa wanafunzi ili kuangalia namna wanavyoendelea na somo.Hali kadhalika, kazi za makundi huandaliwa kwa wanafunzi.

11. ALAMA

Yanayohusika Alama

Mazoezi na kazi nyingine 60%

Mtihani wa mwisho 40%