MAELEZO MAFUPI KUHUSU MADHUMUNI YA SOMO NA YALIYOMO
Moduli hii inashughulikia mawanda mbalimbali ya kufundisha lugha ya Kiswahili ikionyesha umuhimu wake kusaidia mwanafunzi kumudu lugha ya Kiswahili. Moduli hii inajishughulisha vilevile na dhana muhimu za kuandaa somo la Kiswahili kama lugha ya kigeni.
Hali kadhalika, moduli yenyewe inahusika na ubainishaji wa sifa na uonyeshaji wa uhusiano uliopo baina ya Kiswahili na matukio mengine ya kijamii ; inamsaidia mwanafunzi kuchunguza vigezo muhimu vya ubongo (akili) vinavyochangia katika upataji, ufahamu na utoaji lugha.